22 Novemba 2025 - 14:17
Source: ABNA
Ansarullah wa Yemen Waionya Saudi Arabia

Maafisa wa harakati ya Ansarullah ya Yemen wameionya Saudi Arabia kuhusu matokeo ya uchochezi mpya wa vita dhidi ya nchi hiyo, kwa mujibu wa mipango ya Marekani na utawala wa Kizayuni.

Kulingana na shirika la habari la ABNA likinukuu Arabi 21, Abdullah Al-Nuaimi, mjumbe wa Ofisi ya Kisiasa ya harakati ya Ansarullah ya Yemen, alisisitiza kuwa Muhammad bin Salman, Mwanamfalme wa Saudi Arabia, hakujifunza kutokana na mashambulizi ya miaka minane dhidi ya Yemen; mashambulizi ambayo alianzisha na muungano wa Kiarabu, Marekani-Kizayuni wakati Yemen haikuwa na hata kombora moja.

Aliongeza: "Marekani itamtupa Bin Salman katikati ya mapigano haya na kisha kumwacha, kama ilivyomwacha Netanyahu."

Ali Al-Qahoum, mjumbe wa Ofisi ya Kisiasa ya harakati hiyo, pia alisema: "Saudi Arabia inapaswa kukubali ukweli mpya nchini Yemen kama nchi. Mapinduzi ya Yemen yametokana na matakwa ya watu wa nchi hiyo."

Alisema: "Njia ya amani iko wazi, na milango yake iko wazi ikiwa Saudi Arabia ina nia ya dhati ya kufikia amani. Amani inafikiwa kwa kukomesha uchokozi, kukomesha uvamizi, kuondoa mzingiro, kujenga upya maeneo yaliyoathirika, pamoja na kuachilia wafungwa. Ndipo Wayemen wanaweza kutatua matatizo yao katika mazingira tulivu na imara bila uingiliaji wowoni kutoka nje."

Your Comment

You are replying to: .
captcha